OKOA KITAA ni programu inayofanaya kazi na kuendeshwa chini ya taasisi ya maenedeleo ya vijana Tandale, inayolenga kusaidia vijana waishio maeneo duni kwa kutoa elimu ya kujitambua,ujasiliamali na uraia ili kufanya vijana kuwa sehemu ya maendeleo katika jamii na kutimiza ndoto zao . Okoa kitaa imeazishwa mnamo oktoba 2014 kama programu ya kusaidia vijana kwa kutoa elimu katika nyanja ya kijamii,kiuchumi na kisiasa.
OKOA KITAA inalenga kusaidia vijana wa rika lote(wakike na kiume), muda mwingine inagusa ata watu wazima.
Maeneo yanayolengwa zaidi na progaramu hii ni maeneo yenye mzingira duni.
DIRA YA OKOA KITAA
Kuona vijana wanakuwa sehemu ya maendeleo katika jamii na wanasimama katika ndoto na malengo yao na wanafanikiwa kuzitimiza.
DHAMIRA YA OKOA KITAA
Kutoa elimu ya kujititambua, uraia na ujasiliamali kwa vijana wote walio mashuleni na wasio mashuleni.
MALENGO YA OKOA KITAA
Programu ya OKOA KITAA imeanzishwa kwa lengo la kusaidia vijana,na ina malengo yake ili kuanikiawa,malengo hayo ni;
I. Kubadili mwenendo kwa vijana na kuachana na tabia hatalishi zitakazopelekea kushindwa kufikia malengo yao kwa kutoa elimu ya kujitambua kwa ijumla.
II. Kuongeza ushiriki wa vijana katika jamii kwa kuwapa elimu ili watambue hakina wajibu wao katika jamii.
III. Kuboresha na kendeleza mazingira kwa kutoa elimu ya kuifadhi mazingira.
IV. Kupamba na halia ya umasikini kwa vijana kwa kutoa elimu ya kutambua na kutumia fursa ili waweze kubuni mawazo ya kibiashara
SHUGHULI ZA OKOA KITAA
Mpango huu wa okoa kitaa unaendeshwa kwa kuwakutanisha na kuwafikia vijana kupitia;
JUKWAA LA VIJANA; hapa huwa tunakutanisha vijana kutoka sehemu tofauti na kujadili kwa pamoja changamoto zinazowakabili vijana huku tukiangalia njia mbadala za kukabiliaana nazo.
TUONGEE KIJIWENI; hapa tunafanya mazungumzo na kuelimisha vijana kwa kukutana nao kwenye sehemu ambazo vijana wanakutana kila siku kuzungumza mambo yao kila siku.lakini pia vijana wanaweza wakatoa pendekezo la sehemu gani ambayo tunaweza kukaa na kufanya majadiliano nao.
Kauli mbiu yetu ya kuwakutanisha vijana ni TUKUTANE, TUJADILI na TUAMUE.
ZIARA ZA MASHULENI; tofauti na kukutanina au kuwafikia vijana katika mitaa kingine ni ziara mashule hapa uwa tunaenda katika shule za msingi na sekondari kwa lengo la kutoa elimu kwa vijana kuweza kupambana na changamoto anazokumbana nazo kijana katika maisha yake ya kila siku,
Imeandaliwa na
Neman Karan
Muasisi wa OKOA KITAA
+255 674 404 056
Barua pepe: nemankaran@yahoo.com
Neman Karan
Muasisi wa OKOA KITAA
+255 674 404 056
Barua pepe: nemankaran@yahoo.com

No comments:
Post a Comment